Wagombea wakuu wa uchaguzi mkuu nchini Mali
Uchaguzi wa Mali ambao umekuja kufuatia mapinduzi ya
kijeshi pamoja na waasi kuteka sehemu ya Kaskazini mwa nchi, utakuwa na
duru ya pili, kwa mujibu wa tangazo la serikali.
Hii inatokana na ukweli kuwa hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizopigwa ambazo zingemuwezesha kuwa mshindi.
Waziri mkuu wa zamani, Ibrahim Boubacar Keita na
aliyekuwa waziri wa fedha, Soumaila Cisse watatoana kijasho katika duru
ya pili ya uchaguzi itakayofanyika tarehe 11 Agosti.
Uchaguzi unanuia kurejesha demokrasia baada ya zaidi ya mwaka mmoja ya mgogoro wa kisiasa.
Chanzo: BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment