JESHI la Polisi mkoani Ruvuma kupitia kikosi cha usalama barabarani
limewaonya waendesha pikipiki maarufu kwa jina la yeboyebo kuacha mara
moja tabia ya kubeba mizigo isiyosatahili kwenye pikipiki
wanazoziendesha baada ya kubaini kuwa baadhi yao wamekuwa wakibeba maiti
kwenye pikipiki hizo.
Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma mkuu wa
kikosi cha usalama barabarani mkoani humo Severin Mtaki alisema kuwa
hivi karibuni kumeibuka tabia mbaya ya baadhi ya waendesha pikipiki
ambao wamekuwa wakibeba mizigo mizito isiyostahili ikiwa ni pamoja na
kubeba maiti kwani kuna matukio kadhaa ambayo yametokea katika Wilaya za
Tunduru na Nyasa.
Alisema kuwa matukio hayo ya kusafirisha maiti kwa kutumia pikipiki
yamekithiri sana kwenye Wilaya hizo ambapo waendesha pikipiki baadhi
yao tayari wamekamatwa wakiwa wanasafirisha maiti kwa kutumia pikipiki
jambo ambalo jeshi hilo limelazimika kutoa onyo kali kwa waendesha
pikipiki kuacha mara moja tabia hiyo mbaya.
Mtaki alisema kuwa kuanzia sasa askari wa usalama barabarani
wameagizwa kuwakamata waendesha pikipiki watakao kiuka agizo hilo na
kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yao na si vinginevyo.
Alieleza kuwa pikipiki za abiria zimekuwa ni usafiri uliojipatia
umaarufu mkubwa mkoani Ruvuma na ndani ya huduma hiyo abiria wamekuwa
wakifurahia huduma hiyo lakini baadhi ya waendesha pikipiki wamekuwa
wakifanya bihashara haramu ya kusafirisha maiti kwa kuikarisha katikati
mfano wa mshikaki yaani mbele anakaa mwendsha pikipiki katika maiti na
nyuma nakaa mtu mwingine ambaye anaikumbatia maiti jambo ambalo alidai
kuwa ni la atari kwa sheria za usalama barabarani.
Aidha mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Ruvuma Mtaki
alidhibitisha kuwa kunatukio moja alilokutana nalo la pikipiki iliyokuwa
imebeba pikipiki nyingine na juu yake kubeba abiria ambapo aliongeza
kuwa pia ubebaji wa maiti kwa kutumia pikipiki ndio umekithiri sana
ambapo hajajua tatizo hasa ni nini la kusmaiti kwa kutumia pikipiki
jambo ambalo limeifanya jeshi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini
sababu.
Via Songeayetu
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment