Muda wa saa 48 wa kusalimisha silaha kwa waasi wa March 23(M23),
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umemalizika na wakati
wowote mapigano yanaweza kuanza.
Misheni ya Kutuliza Amani ya Umoja wa
Mataifa (Monusco) , ilitoa saa hizo zinazomalizika leo na Jeshi la UN
litaanza kutumia nguvu kunyang’anya silaha waasi hao.
Taarifa iliyotolewa na Monusco iliyotolewa na
Msimamizi wa Misheni hiyo, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos
Cruz na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana,
inaeleza kwamba, watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi ambalo
linajumisha Goma na Sake na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama
wamepewa saa 48 kuanzia saa kumi jana (juzi) kwa saa za Goma (Jumanne)
kuzisalimisha silaha zao.
Taarifa ilisema, “Baada ya saa 10 jioni ya
Alhamisi, Agosti Mosi, wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha
zao watachukuliwa kama tishio kwa usalama wa wananchi na Monusco
itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja na
kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika mamlaka na sheria za ushiriki
za Monusco.”
Kwa mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi
milioni moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kandokando ya
barabara ambayo inawaunganisha na kambi ya wakimbizi ya Mugungu ambayo
ni makazi ya muda ya watu karibu 70,000 ambao wameyakimbia makazi yao
kutokana na mapigano.
Kwa mujibu wa Monusco, tangu katikati ya Mei eneo
hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa Kundi la M23
dhidi ya Majeshi ya Serikali ya FARDC ikiwa ni jaribio la wazi la kutaka
kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.
“Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia kiholela silaha zao za moto zikiwamo silaha nzito ambazo zimesababisha wananchi kujeruhiwa.”
“Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia kiholela silaha zao za moto zikiwamo silaha nzito ambazo zimesababisha wananchi kujeruhiwa.”
Taarifa hiyo imeongeza kwamba kundi hilo la M23 katika mashambulizi hayo limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.
Taarifa hiyo inabainisha kwamba eneo hilo maalumu
la usalama (security zone)litasaidia kudhibiti tishio la moja kwa moja
mbali na eneo la nje ya Goma na pengine eneo hilo linaweza kupanuliwa na
kurudiwa sehemu nyingine kutakako hitajika.
Tamko hilo la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha
silaha zao linafuatia kuwasili katika eneo la Goma kwa Kamanda Mkuu wa
Monusco, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz ambaye
alitangaza kwamba Misheni ya Monusco itaunga mkono Jeshi la
Serikali(FARDC) katika kuanzisha eneo la usalama kuzunguma eneo la Goma
na vitongoji vyake.
Via Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Via Mwananchi
0 comments:
Post a Comment