Mkurugenzi TCRA  Profesa John Nkoma

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imezindua kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya mitandao ya mawasiliano ikiwemo mitandao ya kijamii na simu za mikononi. 

Mkurugenzi TCRA  Profesa John Nkoma amesema mamlaka hayo yameitambua rasmi mitandao ya kijamii kama blogs kama vyombo vya habari ambapo TCRA inaandaa utaratibu kukutana na wamiliki na waandishi wake  kujadili juu ya matumizi mazuri vyombo hivyo vya mawasiliano.

 Mkurugenzi huyo amesema kwa kushirikiana na TCRA watashauriana jinsi ya  kutafuta wataalamu kwa ajili ya kutoa mafunzo mbalimbali juu ya matumizi ya mitandao na ujuzi zaidi katika mawasiliano ya mitandao husika.

Mamlaka hiyo imetoa tahadhari  kwa  wananchi kuwa makini katika kutumia vyombo vya mawasiliano kwani  kutumia mawasiliano vibaya ni makosa kama ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya kielectroniki na posta (EPOCA) ya mwaka 2010.

Profesa Nkoma  amewataka watumiaji wote wa simu za mkononi na wananchi wote kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya sekta ya mawasiliano ambayo huchangia uchumi wa taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Wananchi na  watumiaji wa huduma za mawasiliano wanaarifiwa kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki watoe taarifa kwa vyombo husika, kisha waufute ujumbe huo kwani wakieneza kwa watu wengine watakuwa sehemu ya uhalifu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top