Imeelezwa kuwa jumla ya nyumba 214 za makazi na biashara zimeungua moto toka mwaka 2007 hadi juni 2013 kutokana na miundo mbinu hafifu ya umeme katika jiji la Dar es Salaam na kusababisha vifo na uharibifu wa mali.

Meneja Mawasiliano na uhusiano wa mamlaka ya nishati na maji EWURA Bwana Titus Kaguo amesema miundo mbinu mipya ya umeme na majengo marefu inahitaji wakandarasi mahiri  zaidi vinginevyo inaweza kuleta maafa.

Bwana Kaguo amesema baadhi ya wafanyakazi wanaosuka mifumo ya umeme katika majengo hayo hawana utaalam bali wamekuwa wakiifanya kazi hiyo kwa uzoefu na kuhatarisha maisha ya raia na mali zao.

Uongozi wa EWURA umefafanua kuwa utaendelea kudhibiti ajali hizo kwa sheria ya umeme ya uzalishaji na uzambazaji umeme ya mwaka 2008 ambayo itawabana VISHOKA ambao hawana utaalam stahiki na kudhibiti upotevu wa umeme.

Imeelezwa kuwa wakati Tanzania inaelekea kwenye mfumo wa uchumi wa kati, miradi mingi ya maendeleo inahitaji miundo mbinu imara ya umeme na wataalam waliobobea katika fani hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top