Raia wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa
Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya
udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa miaka 89 amesema atang'atuka ikiwa
yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa.
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha
Movement for Democratic Change (MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa
kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili kunyakua ushindi, lakini
chama tawala kimekanusha madai hayo.Shughuli za kampeini zimekua ghasia
zozote huku kukiwa na visa vichache sana vya kuwatisha wapiga kura.
Vyama vya Zanu-PF na MDC viliunda
serikali ya muungano mwaka wa 2008 baada ya muafaka wa kumaliza ghasia
za baada ya uchaguzi kufuatia matokeo ya Urais yaliyozua utata.
Bw.Tsvangirai alishinda awamu ya kwanza, lakini akajiondoa kwa raundi ya
pili akilalamikia mashambulizi yaliyolenga wafuasi wake.
Serikali ya Zimbabwe imewapiga marufuku
waangalizi wa magharibi kuchunguza uchaguzi wa leo. Hata hivyo Muungano
wa Afrika{AU}, Kanda ya Kusini mwa Afrika{SADC} na makundi ya kijamii
nchini Zimbabwe yamekubaliwa kufuatilia jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa.
Watu milioni 6.4 wamejiandikisha kupiga kura huku maelfu walijitokeza kwenye kampeini za uchaguzi. Matokeo
yanatarajiwa kutolewa kwa siku tano zijazo. Mwandishi wa BBC aliyeko
Harare amesema kuna foleni ndefu katika vituo vya kupigia kura leo ikiwa
siku ya mapumzoko kuhakikisha raia wanapata nafasi ya kuamua serikali
mpya.
Mshindi wa moja kwa moja sharti apate asili mia
50 ya kura zote kutangazwa Rais. Ikiwa hakuna mgombea atapata kura hizo,
raundi ya pili imepangwa kufanyika Septemba 11. Uchaguzi huu ndio wa
kwanza kufanyika Zimbabwe chini ya katiba mpya iliyopitishwa mnamo mwezi
Machi mwaka huu.
Chanzo: BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment