Mashindano ya Riadha ulimwenguni yamefunguliwa hii leo mjini Moscow nchini Urusi.
Takriban wanariadha 2,000 kutoka zaidi ya mataifa 200 wanashiriki.
Haya ndio ya mwanzo kati ya mashindano matatu
yatayofanywa Urusi katika miaka mitano ijayo, pamoja na Olimpiki za
Winter na Kombe la Kandanda la Dunia la mwaka 2018.
Mbio za kwanza za mashindano hayo zitajumuisha
wanariadha mashuhuri kama vile bingwa wa mbio za mita 100 Usain Bolt na
mshindi mara mbili wa mbio za Olympiki raia wa uingereza Mo Farah.
Matayarisho ya mashindano hayo hata hivyo
yamekumbwa na kashfa za baadhi ya wanariadha wanaotumia dawa za
kuzidisha nguvu, huku waandalizi wakisema kuwa watatumia ukaguzi maalum
wa kuwazuia wanariadha watakaotumia dawa hizo.
Chanzo: BBCSwahili
0 comments:
Post a Comment