Profesa Anna Tibaijuka akiongea na wanahabari jijini Dar es Salaam
kuhusiana na utekelezaji wa ujenzi wa Mji mpya wa Kigamboni, Dar es
Salaam
Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amewataka viongozi kuwa
wazalendo na kuacha kuwapotosha wananchi juu ya uendelezaji mradi wa Kigamboni
kwani una umuhimu mkubwa kwa ukuaji wa uchumi wa Watanzania.
Profesa Tibaijuka amesema serikali imejipanga
kuhakikisha inatoa elimu kwa umma kuhusiana na manufaa ya kuendeleza eneo la
mji mpya wa Kigamboni.
Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imefafanua kuwa
mbali na kutoa elimu kwa wananchi,serikali inatafuta fedha za kutosha
kuendeleza mradi na kupima maeneo husika kwa ajili ya kuendeleza mradi huo.
Waziri huyo amesema mji huo utakuwa kitovu cha
maendeleo ya kiuchumi kutokana na fursa za uwekezaji na kulifanya jiji la Dar
es Salaam kushindana miji mingine duniani.
Profesa Tibaijuka amesema hatua nyingine
zinazofanyika ni kufanya tathmini ya mali na kujenga nyumba mpya za kuishi
wananchi watakaohamishwa kupisha mradi wa ujenzi wa mji mpya.
Ujenzi wa mji mpya Kigamboni ni mkakati wa
serikali kukabiliana na ukuaji wa jiji ambao utakuwa na wakazi laki NNE na
uendelezaji huo utafanywa kwa ushirikiano wa serikali na taasisi binafsi.
0 comments:
Post a Comment