SERIKALI inapata mapato ya takribani Sh. milioni 3.5 kwa
siku kutokana na usafiri wa treni katika
jiji la Dar es Salaam.
Aidha Dk. Mganilwa tuzo pia imetolewa kutokana na Waziri Mwakyembe ameweza kufufua na kuweka
kwenye fikra Reli ya Musoma ya kwenda Arusha na Reli Tanga.
Akizungumza katika makadhiano hayo,Dk.Mganilwa amesema kuwa tuzo hiyo ilizingatia vigezo vyote
muhimu vya kumpata mshindi kwa kuzingatia
mchango wa muhusika katika sekta ya hiyo
,mtazamo wa wananchi kwa mtu husika na msimamo binafsi wa mtu husika kwenye uboreshaji huo.
“Ninyi ni mashuhuda
wa mapinduzi ya usafiri wa treni za abiria jijini Dar es Salaam unaowanufaisha
zaidi ya abiria 14,000 kila siku na ikumbukwe kwamba wazo la kuanzishwa usafiri
huo lilikuwepo lakini Mheshimiwa Waziri ndiye aliyekuja kufanya ndoto hiyo kuwa uhalisia”alisema
Dkt.Mganilwa.
Tuzo hiyo imepatikana baada ya kushindanishwa kwa majina
matatu ya watu ambao wana mchango mkubwa kwenye maendeleo na mapinduzi ya reli
Tanzania kwa kurejea kila mmoja katika kipindi chake cha na kile alichokifanya.
Aidha ameiomba Serikali kupitia wizara ya hiyo kuanzisha
mfuko wa miundo mbinu kwa fedha zitakazo kuwa zinapatikana katika usafirshaji ili
kuweza kuendelea kuboresha suala hilo na kukuza uchumi wa nchi yetu pamoja na kuleta
maendeleo.
Naye Waziri Mwakyembe ameishukuru kampuni hiyo kwa kuuona mchango wake katika jamii na
kuweza kumpatia tuzo, ambayo ni motisha itakayo
muongezea juhudi za kuliletea Taifa letu maendeleo kupitia sekta ya hiyo.
“Kwa niaba ya TRL, RHACO na wafanyakazi wote wa wizara ya
Uchukuzi napenda kuishukuru kampuni ya
Mwandi Tanzania kwa kuuona mchango wangu katika sekta ya usafiri wa treni bado
tunaendelea kuweka mipango madhubuti kuboresha usafiri wa treni nchini na
Afrika Mashariki kiujumla”alisema Dkt.Mwakyembe.
Watu wengine walioshiriki katika ushindani wa tuzo
hiyo, Injia Festo Mwanyika na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Reli Tanzania na Linford Mboma kutoka Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA).
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment