Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akiingia katika viwanja vya stendi ya malori mjini songea ili kuzungumza na wananchi.
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akihutubia wananchi jana katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini uliofanyika katika viwanja vya stendi ya malori mjini Songea. |
Wananchi wakifuatilia hotuba ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya stendi ya malori mjini Songea jana.
Kila
mtu alijitahidi kupata nafasi nzuri ili aweze kufuatiliwa vyema matukio
mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano huu kama
inavyoonekana.Njiwa walirushwa kuonesha ishara ya upendo wakati wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini ya Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Mwenyekiti
CHADEMA taifa, Freeman Mbowe akihutubia wanachama wa CHADEMA katika
mkutano wa kuchagua viongozi wa chama Kanda ya Kusini ya mikoa ya Lindi,
Mtwara na Ruvuma uliofanyika katika ukumbi wa Heritage Cottage mjini
Songea.
Mwenyekiti
wa taifa CHADEMA, Freeman Mbowe akimkabidhi Mwenyekiti mteule wa CHADEMA
Kanda ya Kusini katiba ya CHADEMA ambayo atapaswa kuilinda na kuitetea
wakati wa uongozi wake.
Mwenyekiti
wa CHADEMA kanda ya kusini, Mwalimu Joseph Matiko akizungumza katika
mkutano wa wanachama wa CHADEMA kanda ya kusini (hawapo pichani) ambapo
aliwashukuru kwa kumchagua na akaahidi kuitekeleza majukumu yake kwa
mujibu wa katiba ya CHADEMA. Kushoto ni Makamu mwenyekiti kanda ya kusini Lusajo Mwangupili.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akimtakia kila la heri Mwenyekiti wa kanda ya Kusini Joseph Matiko. Kushoto ni Makamu mwenyekiti kanda ya kusini Lusajo Mwangupili.
Mwananchi mmoja, aliyejitambulisha kw a jina laWilly Migodela (Kulia), akiwasomea wananchi kipengele cha mwaka 2006 katika katiba ya CHADEMA kuhusu uhalali na wajibu wa vikundi vya Red Brigade katika chama kikatiba.
Mbunge
wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa akihutubia wananchi
katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi Kanda ya kusini uliofanyika mjini
Songea jana.
Viongozi
mbalimbali wakitoa salam kwa wananchi wakati katika mkutano wa uzinduzi
wa Kanda ya Kusini ya mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma uliofanyika
katika viwanja vya Stendi ya Malori mjini Songea.
Picha zote na Azimioletublog
0 comments:
Post a Comment