Imeelezwa kuwa iko haja ya Serikali kuandaa mitaala ya
pamoja katika Skuli za maandalizi ili kuepuka kutofautiana kiuwezo wa
elimu kwa wanafunzi wa Skuli za Serikali na Skuli za Kibinafsi.
Wamesema elimu ya maandalizi ni
msingi wa kumuezesha mtoto kujiandaa ili akianza elimu ya
msingi aweze kuwa na ufahamu mzuri.
Wajumbe wa baraza la wawakilishi
wameeleza hayo wakati wakichangia Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
Mbweni nje kidogo na mji wa Zanzibar .
Aidha wawakilishi hao
walisema pamoja na mitaala ya masomo pia wameishauri Wizara ya elimu kuandaa
mitaala ya michezo ili kuweza kukuza kiwango cha michezo
nchini.
Wakizungumzia suala la
hatimiliki, wachangiaji hao walisema kuna skuli nyingi za Unguja na
Pemba hazina hatimiliki licha ya kwamba baadhi ya skuli hizo zina
umri wa miaka mingi .
Aidha walisema kuwa iko haja ya
kuandaliwa vifaa kwa ajili ya elimu mjumuisho na walimu wanaosomesha masomo
hayo waangaliwe kwa maslahi kwani wanakabiliana na kazi ya ziada katika
kufundisha wanafunzi hao .
Aidha walisema Wizara ya Elimu
imeajiri walimu 578 katika kipindi cha mwaka huu lakini hadi sasa
walimu waliomaliza mwaka 2008 hawajapata ajira.
Wakieleza changamoto
zilizojitokeza ni ukosefu wa walimu katika wilaya za Pemba.
Wete.Chakechake na mkoani.
Wakifahamisha kwamba walimu
wanaopata ajira wazingatiwe na wilaya zao wanazoishi kwa
kurahisishiwa masafa.
Aidha walieleza kuwa walimu
hawafanani na chochote hivyo wanahitaji kuenziwa kutunzwa na kuthaminiwa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment