MWANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Tegeta, Dar es Salaam, Mpesa Amri
(15) amefariki dunia kwa kujinyonga kwa madai ya kuhimizwa kuhusu
masuala ya shule.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema jana
kuwa tukio hilo lilitokea Julai 16 mwaka huu, majira ya saa 11 jioni,
maeneo ya Tegeta Namanga.
Alisema chanzo cha tukio hilo ni mzazi wake, Agilina Maiko kumuhimiza
juu ya kufanya maandalizi ya shule ambazo zimefunguliwa hivi karibuni.
“Baada ya mama mzazi kumwambia kuhusu shule huku yeye akiwa hataki
tena habari za kusoma na badala yake kufanya kazi, mwanafunzi huyo
alichukua uamuzi huo,” alisema ingawa hakubainisha ni kazi gani alikuwa
anapenda kufanya.
Polisi wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Katika tukio jingine, Richard Dustan amefariki dunia baada ya pikipiki
T 134 SKM Boxer aliyokuwa akiendesha kugongana na gari T 533 AGA
aina ya Scania.
Ajali hiyo ilitokea jana, maeneo ya Ubungo- External. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment