Naibu waziri mkuu wa Mambo ya nje Marekni William Burns
Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani William
Burns amewasili mjini Cairo Misri tayari kwa mkutano na viongozi wa
serikali ya mpito wanaoungwa mkono na jeshi.
Ni Ziara ya kwanza kufanywa na afisaa mkuu wa
Marekani tangu jeshi kumwondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohamed Morsi
tarehe 4 Julai.
Duru kutoka Ikulu ya rais Marekani,
zinasema kuwa Burns atashinikiza kumalizwa kwa ghasia na vurugu na
kuundwa kwa serikali ya pamoja ya viongozi wa kiraia watakaochaguliwa
kidemokrasia.
Awali mwendesha mashtaka mkuu alipiga tanji mali za viongozi 14 wa kiislamu.
Kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood
Mohammed Badie na naibu wake Khairat al-Shater wanaripotiwa kuwa
miongoni mwa waliokamatwa.
Hatua hiyo ni sehemu ya uchunguzi kuhusu madai ya uchochezi, yaliosababisha ghasia za kisiasa nchini humo.
Mamia ya watu wamefariki wakati wa maandamano
yaliyofanywa na mahasimu wa kisiasa kati ya wale wanaomuunga mkono Morsi
na wapinzani wake, katika wiki mbili zilizopita.
Wakati huohuo maafisa wanasema kuwa washukiwa wa
chama cha Brotherhood, wameshambulia basi lililokuwa linawabeba
wafnyakazi wa kiwandani Kaskazini mwa Sinai huku wakiwaua watu watatu.
Chanzo: BBC Swahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment