Imezoeleka katika jamii, hasa kwa wanasiasa, kuwa na kauli ya "Mwanamke akiwezeshwa anaweza" kwa imani kuwa bila nguvu za ziada kufanyika mwanamke hawezi kufanya chochote cha kumletea maendeleo.

Kauli hii inaonekana haiko hivyo kwa wanawake wote kutokana na kilichonaswa na kamera yetu katika eneo la Hospitali ya Rufaa Mbeya siku ya Ijumaa (12.07.2013) ambapo akina dada wawili walionekana wakifanya kazi ya kufyatua tofali kwa hiari yao wenyewe kazi ambayo imezoeleka kufanywa na wanaume.

Muda wote walionekana wakishiriki kuchanganya udongo na kufyatua tofali ambazo zilikuwa ziliwekwa umbali wa mita zipatazo 30 kutoka eneo la la udongo wa kufyatualia.

Wanawake wa aina hii wanaipa jamii ujumbe kuwa ukombozi wa mwanamke unaanzia kwa mwanamke mwenyewe maana kama mwanamke hayupo tayari kufanya kazi kuwezeshwa hakuna maana maana yoyote.

Bahati mbaya chanzo chetu hakikufanikiwa kuzungumza na wahusika kwa vile mazingira hayakuruhusu.

Na azimioletublog
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top