Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja(Kaunda suti nyeusi) akimtambulisha Mhe. Waziri wa Uchukuzi, Dkt.
Harrison Mwakyembe kwa Wakuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga
na Mkoa wa Mara baada ya kuwasili mapema asubuhi katika Uwanja wa ndege
wa Mwanza tayari kwa Ziara ya Kikazi katika Magereza Mkoani Mwanza leo
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja(aliyepo kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng.
Evarist Ndikilo( aliyepo kulia) mapema leo Julai 23, 2013 alipofika ofisini
kwake kuweka sahihi katika Kitabu cha Wageni(mwenye shati jeupe) ni Kamishna wa
Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja(suti nyeusi) akiangalia Mashine Maalum ya kupimia Magonjwa
mbalimbali wakati alipomtembelea Zahanati ya Gereza Butimba mapema leo Julai
23, 2013, anayeelezea ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Mariam Lumuli ambaye ni
Mtaalam wa Maabara wa Zahanati hiyo.
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Mwanza
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amewataka Maafisa na
Askari wa Jeshi la Magereza Nchini kuzingatia Taratibu za kazi za kila
siku katika Uendeshaji wa Magereza(Prisons Routine).
Kamishna
Jenerali wa Magereza John Minja ameyasema hayo leo wakati wa Ziara yake
ya Kikazi katika Magereza Mkoani Mwanza alipokuwa akiongea katika
Baraza la Makamanda na Askari wa Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza na
Gereza Butimba, Mwanza.
Pia
Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa Makamanda na Askari watakao
tenda kazi zao kwa ufanisi unaopimika watapandishwa vyeo ili kuwaongezea
molari zaidi ya kazi ambapo amewataka wajitahidi zaidi kutenda kazi zao
kwa weledi katika maeneo yao ya kazi.
Aidha
amewatadhalisha Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Nchini kuacha
mara moja tabia ya kutumia nguvu kazi ya Wafungwa katika shughuli
binafsi kinyume na taratibu za Uendeshaji wa Jeshi la Magereza.
"Tutaendelea
kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na Askari watakaothibitika
kutumia vibaya nguvu kazi ya Wafungwa kwa maslahi yao binafsi".
Alisisitiza Kamanda Minja.
Kamishna
Jenerali Minja pia amezungumzia mafanikio mbalimbali yaliyofanyika
ndani ya Jeshi la Magereza tangu ateuliwe na Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Kamishna Jenerali
wa Magereza.
Ametaja
mafanikio hayo katika Jeshi ni pamoja na kukamilika kwa Karakana ya
kutengeneza Magari katika Gereza Kuu Ukonga, Usajili wa Namba mpya za
Magari ya Jeshi la Magereza, Kuanzishwa kwa Huduma za Maduka yanayouza
bidhaa zisizo na Tozo la Kodi(Duty Free Shops) katika Mkoa wa Dar es
Salaam na Dodoma pia ujenzi unaendelea katika Mikoa ya Morogoro na
Kilimanjaro.
Mafanikio
mengine ni pamoja na kukamilika kwa Jengo la gorofa kwa ajili ya
makazi ya askari wa Magereza Mkoani Iringa, upanuzi wa Zoezi la
Usafirishaji wa Mahabusu kutoka gerezani kwenda Mahakamani katika Mikoa
ya Pwani, Arusha na Mkoa wa Dodoma ambapo zoezi linaendelea vizuri bila
matatizo yeyote.
Kwa
upande wao Maafisa na Askari wa Mkoa wa Mwanza wamempongeza Kamishna
Jenerali kufanya Ziara yake Mkoani Mwanza ili kuweza kujionea changamoto
mbalimbali zinazowakabili pamoja na kusikiliza shida mbalimbali za
Maafisa na Askari.
"Tunampongeza
sana Kamishna Jenerali Minja kwa uamuzi wake wa kuja hapa Magereza
Mkoani Mwanza hasa kuja kuzungumza na sisi Askari wa Magereza Mkoa wa
Mwanza tunaimani kubwa shida zetu zitapatiwa ufumbuzi kwa wakati kama
ilivyokatika Utendaji wake wa kazi kuwa wa kasi na viwango". Alisikika
Askari Mmoja wa Gereza Butimba, Mwanza.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir
Minja kufanya Ziara yake ya kikazi tangu ateuliwe rasmi tarehe 25
Septemba, 2012 kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment