Catherene Aston na Rais wa muda Adly Mansur
Mkuu wa sera ya kigeni katika Muungano wa Ulaya, Catherine Ashton, amekutana na Rais aliyeng'olewa mamlakani Mohammed Morsi.
Msemaji wa Bi Catherene Ashton, alisema kuwa
mkutano ulifanyika katika eneo lisilojulikana ambako Morsi anazuiliwa na
kuwa ulidumu kwa masaa mawili lakini hakutoa maelezo kuhusu walichokijadili.
Bi Ashton aliyewasili mjini Cairo siku ya Jumapilia, anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari baadaye leo.
Hata hivyo, tayari ameshakutana na maafisa kadhaa
wa serikali akiwemo rais wa muda Adly Mansour, mkuu wa majeshi,
Generali Abdel-Fattah al-Sisi na makamu wa rais wa maswala ya
kigeni, Mohamed ElBaradei. Alisema kuwa atatoa wito kwa pande zote mbili
kuhusishwa katika serikali.
Chanzo: BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment