Ili kusonga mbele, sasa Taifa Stars italazimika kushinda mechi zake
mbili za mwisho, dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa Dar es Salaam, kabla
ya kusafiri kwenda Gambia.
Katika mchezo huo, Stars ilihitaji ushindi ili
kujiweka kwenye mazingira mazuri, lakini ilijikifungwa mabao hayo
mawili, moja katika kila kipindi, huku bao la kufutia machozi likifungwa
na Amri Kiemba.
Matokeo hayo, yameifikisha Morocco pointi tano,
lakini ikiendelea kubaki nafasi ya tatu, na Stars imebaki na pointi sita
nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast iliyoifunga Gambia mabao 3-0 na
kufikisha pointi 10.
Kipindi cha kwanza kilishuhudia Taifa Stars
ikipelekwa puta na wenyeji wao waliotawala sehemu kubwa ya kiungo na
hivyo kuruhusu mashambulizi mengi yaliyomnyima nafasi ya kupumzika kipa
na nahodha Juma Kaseja.
Stars ilimtumia mshambuliaji mmoja mbele, Thomas Ulimwengu na kufanya mashambulizi ya kushitukiza langoni mwa wapinzani wao.
Morocco wangeweza kufanya matokeo kuwa tofauti
katika dakika za 5, 9 na 13 kama siyo Yousef El Arab, Hermach na Barrada
kushindwa kumtungua kipa wa Stars.
Stars uliyokuwa ikishangiliwa na mashabiki 300,
walibisha hodi lango la Morocco dakika ya 20 baada ya beki Shomari
Kapombe kumjaribu kipa wa Morocco, Nadir Lamyaghri kwa shuti la mbali
lililopaa juu ya lango.
Dakika tano baadaye Ulimwengu, alikuwa kwenye
wakati mzuri wa kuipatia bao Stars baada ya kupokea mpira mrefu na
kukimbia nao mpaka ndani ya boksi la hatari lakini akapiga kiki dhaifu
iliyodakwa na Lamyaghri.
Mfumo wa Stars kucheza kwa kujiami zaidi kuliko
kushambulia uliendelea kuleta hali ya mashaka langoni mwao, ambapo
dakika ya 38 Morocco walipata bao la kuongoza kwa kiki ya penalti.
Penalti hiyo iliyokwamishwa wavuni na Abderazak
ilitokana na faulo ya beki wa Stars, Aggrey Morris aliyemwangusha ndani
ya dimba la hatari mshambuliaji Issam el Edoua.
Morocco alitumia mwanya wa Stars kucheza pungufu
na kufanya, ambapo mwanzoni mwa robo ya kipindi cha pili, waliongeza bao
la pili kupitia kwa Yousef aliyepita katikati ya ngome ya Stars na
kumpiga chenga Kaseja.
Stars waliibuka dakika ya 60 baada ya kiki kali ya kiungo Amri
Kiemba nje ya 18 kwenda moja kwa moja kutikisa kamba za Morocco na
kufanya matokeo kuwa mabao 2-1.
Baada ya bao hilo, Stars ilionyesha uhai na
kufanya mashambulizi langoni mwa Morocco pamoja na kucheza pungufu
sehemu kubwa ya mchezo huo.
Udhaifu mkubwa wa mabeki wa Stars ulikuwa
kushindwa kucheza mipira krosi, ambayo mingi iliwakuta peke yao
washambuliaji wa Morocco ambao ukosefu wao wa umakini uliwanyima ya
mabao ya wazi.
Stars: Kaseja, Aggrey Morris,
Kelvin Yondan, Frank Domayo, Ngassa/Nadir, Erasro Nyoni, Salum
Abubakar/Khamis Ncha, Ulimwengu/Bocco, Kapombe, Samata, Kiemba.
Mwananchi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment