Kocha mkuu wa Manchester United,  Sir Alex Ferguson.
 
Kocha mkuu wa timu ya Manchester United,  Sir Alex Ferguson ametangaza rasmi kustaafu mwisho wa msimu huu wa ligi kuu nchini England.

Taarifa iliyotolewa na mtandao wa klabu hiyo umedokeza kuwa mechi ya mwisho kwa kocha huyo mwenye mafanikio kukalia benchi la ufundi itakuwa ni kati ya Man United  na West Bromwich Albion.
Hata hivyo kocha huyo anafikiriwa kubakishwa kuwa miongoni mwa viongozi katika bodi ya timu na kuendelea kuwa balozi wa kudumu wa klabu hiyo.
Kocha huyo mwenye miaka 71 amesema kuwa huu ni wakati muafaka kwake kuachia ngazi kwani amefanya mengi katika mchezo wa soka ambapo ameipatia Man United vikombe vipatavyo 30  vikiwemo 13 vya ligi kuu na mabingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya mara mbili.ifuatayo ni orodha ya mkusanyiko wa vikombe alivyochukua kocha Ferguson akiwa old Trafford.

LIGI KUU 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013

KOMBE LA FA : 1990, 1994, 1996, 1999, 2004

KOMBE LA LIGI(CARLING/CAPITAL): 1992, 2006, 2009, 2010

LIGI YA MABINGWA ULAYA : 1999, 2008

KOMBE LA WASHINDI : 1991

KLABU BINGWA YA  DUNIA: 2008

UEFA SUPER CUP : 1991

Inter-Continental Cup: 1999

NGAO YA JAMII/HISANI : 1990 (shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011


Nahodha wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England Bryan Robson amemzungumzia kocha Ferguson kama kocha mahiri ambaye hajapata kutokea katika klabu hiyo na England kwa ujumla.

Haya sasa kufa kufaana wakati kocha Ferguson akitangaza kubwaga manyanga tayari makocha mbalimbali wameanza kupigiwa chapuo akiwemo David Moyes wa Everton ya England huku baadhi ya wakosoaji wakidai huenda akashindwa kazi hiyo kutokana na presha ya mashabiki ambao wamezoea mafanikio.

Kocha Jose Mourinho wa Real Madrid ya Hispania pia ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kutaka kurithi mikoba ya Ferguson huku uvumi ukichagizwa na uhusiano mbovu na mashabiki na uongozi wa miamba hiyo ya Santiago Bernabeu
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top