Mtandao wa jinsia hapa nchini TGNP kwa kushirikiana na wanaharakati wengine wa masuala ya jinsia, ukombozi wa wanawake na haki za binadamu  , umezindua ilani ya madai ya wanawake wa Tanzania katika katiba mpya, ambapo yamo mapendekezo ya madai ishirini na mbili katika kuhakikisha katiba mpya inayoundwa inakuwa katika misingi ya haki na usawa.


Kati ya madai hayo lipo suala la afya ya uzazi , ambapo baadhi ya wanaharakati wamesema afya ya uzazi kwa mwanamke haijapewa kipaumbele huku pia wakilalamikia bajeti ambayo inatengwa kwa ajili ya sekta hiyo.


Madai mengine ni pamoja na masuala ya mirathi kwa wanawake ambapo imebainika wanawake wengi hupoteza muda mwingi katika kufuatilia  mirathi na hivyo kushindwa kujishughulisha na kazi zingine za kimaendeleo.


Hapo awali akizindua ilani hiyo naibu waziri wa katiba na sheria Angella Kairuki amesema kuzinduliwa kwa katiba hiyo ni hatua muhimu katika harakati za kuleta usawa wa kijinsia na kujenga jamii huru.


Serikali ya Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kumwezesha mwanamke ikiwa ni pamoja na kumpatia  fursa mbalimbali  za kimaendeleo na nafasi tofauti za kimaamuzi ingawa bado mwanamke anakabiliwa na changamoto nyingi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top