Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo.

Habari kutoka kutoka Jijini Arusha zinasema kwamba kitu kinachosadikika kuwa bomu kimelipuliwa katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Josefu parokia ya Ora City jijini Arusha na kusababisha maafa. 

Msemaji kutoka katika eneo la tukio ameiambia blog hii ya azimioletu.blogspot.com kuwa ameshuhudia miili ya majeruhi, baadhi yao wakiwa katika hali mbaya, ikiokolewa na kupelekwa hospitalini huku eneo la tukio likiwa limetapakaa damu.
Inasemekana kuwa awali kitu kilitupwa katikati ya watu kanisani na kusababisha kelele  kabla ya kulipuka wakati Balozi wa Papa nchini, Francisco Padla, akiwa katika misa.
Vyanzo tofauti vya habari kutoka eneo la tukio vimeiambia blog hii  kuwa watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.
Inasemekana mshukiwa wa kwanza amekamatwa katika eneo la tukio na mwingine amekamatwa baada ya kukimbia kutoka eneo la tukio.
Inasemekana mshukiwa wa pili alikimbia, lakini mungu mkubwa, alijificha katika nyumba ya mtu na kukutwa humo wakati watu wanamfuatilia kwa vile awali kuna raia waliomwona anapoingia katika nyumba hiyo ambayo cha kushangaza ni kuwa mwenye nyumba alikana kuwa na mtu kama huyo katika nyumba yake, jambo lililowafanya watu wenye hasira kuamua kumtoa kwa nguvu na kuanza kumshushia kipigo.
Kwa upande mwingine polisi wakiwa na mbwa wao waliweza kumfuatilia mshukiwa hadi eneo alikojificha na kumkuta  yuko taabani baada ya kipigo, kisha wakamtia mbaroni.
Awali inasemekana watu wawili walifika katika eneo la kanisa na kurusha kitu katikati ya watu kanisani ambacho kililipuka na kusababisha maafa hayo mnamo majira ya saa 5.30 asubuhi.
Vyombo vya usalama tayari viko katika eneo la tukio kwa usalama zaidi.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top