Imezoeleka kusikia Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli akitoa maagizo kwa wakandarasi waliojenga barabara au madaraja chini ya kiwango kuwa warudie upya kwa gharama zao. 

Blog ya azimioletu.blogspot.com ililikuta daraja moja lililojengwa na kukamilika ujenzi wake mwaka 2012 katika kijiji cha Iwowo, kata ya Itawa Mbeya Vijijini. Wadau mnasemaje juu ya daraja hili? 
Hili ni daraja lililojengwa katika mto Songwe Wilaya ya Mbeya Vijijini, kata ya Itawa kwenye Kijiji cha Iwowo ambalo lilikamilika ujenzi wake mwaka 2012.

Magogo makubwa yametumika kujengea daraja hili na haijulikani yalikotolewa ambako  mazingira hayakuathirika, vilevile,  magogo haya kama yalikuwa katika mpango wa ujenzi wa daraja hili.
Daraja jipya likiwa limejengwa katika nguzo za daraja la zamani, labda, bajeti ya ujenzi wa nguzo mpya haikuwekwa katika bajeti ya ujenzi wa daraja hili kwa makusudi maalumu.
Baadhi ya sehemu za daraja zinaonekana kuwa na nyufa
Inaonekana kuwa watu na gari hupita upande mmoja wa daraja wakati wa kuingia, kuvuka na hata kutoka darajani kutokana na ubovu wa sehemu moja ya kuingilia au kutokea darajani.

Daraja likionekana kwa mbal
Hii ni sehemu ya kijiji cha Iwowo ambako daraja limejengwa.

 PICHA NA BLOG YA AZIMIO LETU

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top