Makampuni
nchini China yameingia katika shutuma kali kua wanatengeza na
kusafirisha vifaa vya mateso kwa vikosi vya polisi duniani.
Shirika
la kutetea haki za binaadamu Amnesty International limetoa taarifa kuwa
makampuni yapatayo mia moja na thelathini nchini humo,kati yao wamekiri
kutengeneza vifaa hivyo ikiwemo vibanio vya umeme,viti vya umeme,na
pingu za vidole gumba.
Inasemekana vifaa vingi japo hutengenezwa na kusafirishwa,vingi matumizi yake ni katika kuleta maumivu mwilini na mateso.
Shirika
hilo la kutetea haki za binadamu lina shaka na nchi zenye ukiukwaji
mkubwa wa haki za binaadamu hasa Africa na Kusini Mashariki mwa Asia wao
ndio wateja wakuu wa vifaa hivyo.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment