Rais
wa Marekani Barack Obama amesema Marekani itashambulia kundi
linalojiitaa Islamic state kote nchini Syria na Iraq ili kuwanyima
kabisa makao ya kujificha .
Bwana Obama amesema kushiriki kwa mataifa
kadhaa ya kiarabu katika mapambano hayo kunaonyesha wazi hivyo si vita
vya Marekani pekee bali wao ni sehemu ya muungano wa mataifa
yanayopigana na kundi hilo liitwalo pia ISIL.
Vilevile amekiri kuwa
mashambulio hayo yamelenga pia wale aliowatajwa kuwa wanamgambo sugu wa Al Qaeda wa kundi liitwalo Khorasan ambao anasema wanalenga kuishambulia
Marekani.
Nazo taarifa za jeshi la Marekani zinasema malengo ya mashambulio yaliyofanywa yametimia.
Wanamgambo kadhaa wa IS wameripotiwa kuuliwa japo vifo vya raia pia vimeripotiwa.
Mapema
msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Alexander Lukashevichy
amesema mashambulio yoyote dhidi ya ISIL ni sharti yazingatie sheria za
kimataifa.
Kadhalika Obama, amesema kuwa kuhusika kwa nchi za
kiarabu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Syria
ni dalili tosha kuwa vita hivi sio vya Marekani pekee.
Obama amesema ataendelea kukusanya jeshi la kimataifa dhidi ya wapiganaji hao.
Saudi Arabia, Milki za kiarabu, Jordan na Bahrain zote zilituma ndege za kijeshi katika operesheni hiyo.
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment