Sekta ya usafiri wa Anga inakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo Miundo  mbinu ya usafiri wa anga hivyo inahitajika kuboreshwa ili kuwasaidia wawekezaji kupanua huduma za usafiri kwa wananchi.
Katibu mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma za  usafiri anga Bwana Hamza Johari amesema Uhaba wa viwanja na wataalam ni miongoni mwa changamoto inayorejesha nyuma maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.
Katibu huyo amesema kukosekana kwa ushindani wa makampuni makubwa katika sekta hiyo yanafanya usafiri kuwa ghali kutokana kutokuwa na ushindani kwani wanajua wananchi lazima watapanda ndege zao
Baraza la watumiaji wa huduma za usafiri wa Anga Tanzania limewataka wadau kuunga mkono jitihada za baraza ili kuleta nafuu  katika usafiri husika.
Katibu huyo  amesema lengo kubwa la baraza hilo ni kutetea haki za watumiaji huduma hivyo wataendelea kuwaelimisha kwa semina na warsha.
Katibu huyo amesema licha ya hamasa ndogo ya watanzania katika usafiri wa anga,mwamko umeanza kuonekana kutokana na kuelimishwa na baadhi ya makampuni yameanza kujitoa huduma kwa bei nafuu zaidi.
Bwana Hamza amesema miongoni mwa mikakati ya baraza hilo ni kuwafikia wananchi wa kipato cha chini  kwa hivi sasa huduma za usafiri wa anga zinaonekana ni za watu wa kipato cha juu na cha kati.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top