Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imezitaka
kampuni zote zilizopewa leseni za kuuza ving’amuzi kuongeza ubora wa matangazo
yao ili kukidhi matarajio ya kuhamia mfumo mpya wa digitali
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Prof John Nkoma amesema kampuni hizo
zinatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni ambazo ziliwapatia
leseni ya kufanyia biashara kwa viwango vinavyotakiwa.
Mkurugenzi huyo amezitaka kampuni hizo kutanua
wigo wa shughuli zao kwa kufungua na kuongeza sehemu za mauzo ili kukabiliana
na wimbi kubwa la wateja wanaohitaji huduma na kutatua matatizo yanayojitokeza
mara moja.
Aidha Profesa Nkoma ameviagiza vituo vya Luninga
ambavyo havijajiunga na mfumo wa digitali kufanya hivyo mara moja ili kufikisha
huduma kwa wananchi kwa wakati.
Mamlaka hiyo inaamini kuwa utangazaji wa
Televisheni kwenye mfumo wa Digitali utakuwa chachu kubwa kwa ukuaji wa uchumi
wa nchi na kuwaomba wananchi kujiunga kwa haraka katika mfumo huo mpya.
0 comments:
Post a Comment