RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein ameeleza haja kwa Serikali ya India kurejesha utamaduni
uliokuwa ukifanya miaka ya nyuma wa kuwaleta madaktari bingwa kwa zamu hapa
Zanzibar hatua ambayo ilisadia sana kuimarisha sekta ya afya
Dk. Shein aliyasema hayo
wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi mdogo wa India Pawan Kumar ambaye alifika Ikulu mjini
Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.
Dk. Shein amesema kuwa mnamo miaka ya 1970 hadi mwanzoni
mwa miaka ya 1980, India ilikuwa na utaratibu huo wa kutela madaktari bingwa
visiwani Zanzibar ambao waliweza kufanya kazi na kutoa huduma za afya kwa
wananchi hatua ambayo ni busara kuanzishwa tena ili kuendeleza kuimarisha sekta
ya afya hapa Zanzibar.
Katika maelezo yake Dk. Shein amesema kuwa kuwepo kwa
madaktari bigwa hapa nchini kutoka India kutasaida zaidi kuimarisha huduma
katika hospitali za Zanzibar hasa hospitali za Wete na Chake kisiwani Pemba
ambazo kwa hivi sasa zina upungufu wa madaktari bigwa.
Mbali na hatua hiyo, Dk. Shein amesisitiza umuhimu wa
kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa madatari wa India na Zanzibar kwa awamu,
juhudi ambazo zitasaidia kuipinguzia gharama Serikali ya kupelekea wagonjwa
katika hospitali zilizopo nchini humo.
Dk. Shein ameeleza kuwa India ni miongoni mwa nchi
zilizopiga hatua katika kufanya utafiti wa kilimo hivyo alieleza haja ya
kuimarisha ushirikiano katika sekta hiyo hasa kwa kushirikiana na wataalamu wa
Kitengo cha Utafiti wa Kilimo kiliopo Kizimbani.
Naye Balozi huyo mdogo wa India amemueleza Dk. Shein kuwa
nchi yake itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo ambao ni wa muda mrefu na
umekuwa na historia kubwa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment