WANANCHI wametakiwa kuendelea kuiamini Serikali na viongozi wake na kuepuka kulaumiana badala ya kushikamana katika kukabiliana na changamoto za maendeleo zinazolikabili taifa.
Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza na wakulima wa bonde la Kilombero huko Mwembe Mpunga wilaya ya Kaskazini ‘B’ mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais alifika katika bonde hilo kukagua athari za jua kwa kilimo cha mpunga katika bonde hilo katika siku yake ya pili ya ziara ya siku mbili kutembelea mkoa huo.

Katika maelezo yao kwa Rais wakulima hao walieleza kutoridhishwa na kiwango kidogo cha madawa ya kuulia magugu wanachopewa, huduma hafifu za matrekta na kutokupatikana kwa wakati mbegu za muda mfupi.

Aliwahakikishia wananchi hao kuwa azma na dhamira ya serikali ya kufanya mapinduzi ya kilimo ni thabiti na imeanza kutekelezwa kwa vitendo ambapo hatua mbalimbali zimechukuliwa kutekeleza azma hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top