Waandishi wa habari wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mabaraza ya kutoa maoni ya katiba mpya.

Mkurugenzi wa kituo cha Haki za binadamu LHRC Dakta Hellen Kijo Bisimba amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuhamasisha wananchi katika mchakato mzima wa uundwaji wa katiba mpya kupitia mabaraza husika.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa masuala ya haki za wanawake kwa sababu wamekuwa wakikandamizwa kwa muda mrefu lakini zinapuuzwa hivyo kuna umuhimu wa kuwekwa bayana katika katiba mpya.

Kutokana na mchango wa vyombo vya habari na kushirikishwa kwa wananchi katika mchakato huo kuna matumaini makubwa ya kuipata katiba ambayo kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakiihitaji.

Kituo hicho kimeandaa siku mbili za mafunzo kwa wanahabari kuhusiana na haki za wanawake kwenye katiba na ushiriki wa vyombo vya habari  kwenye mabaraza ya  katiba.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top