Serikali imeishukuru serikali ya Saudi Arabia kwa kutoa vifaa vya kisasa vya kufanyia upasuaji na masuala mbalimbali ya afya katika kitengo cha mifupa cha Moi cha hospitali ya Muhimbili.
Akongea baada ya kupokea msaada huo kutoka kwa ujumbe maalumu kutoka Saudi Arabia, waziri wa Afya nchini Dr Hussein Mwinyi amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa upasuaji wa watoto wenye matatizo ya kuzaliwa na vichwa vikubwa pamoja masuala mengine.
Naye balozi wa Saudi Arabia, Hani Monimal, ambaye ndiye aliyeongoza msafara wa maafisa kutoka nchini kwake ameahidi nchi yake kuendelea kutoa misaada nchini hususa katika sekta ya afya.
Vifaa vingi vilivyokabidhiwa ni vile venye uwezo wa kukabiliana na tatizo la watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa ambapo tafiti zinaonesha kuwa kila mwaka zaidi ya watoto elfu nne huzaliwa na tatizo hilo hapa nchini.






TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top