Jukwaa la wahariri nchini limesema linaamini kushambuliwa kwa mwenyekiti wa jukwaa hili Absolum Kibanda halijafanywa na majambazi bali na kikundi cha watu wenye nia mbaya ya kuzuia majukumu yake ya kazi ya kila siku.
Teophil Makunga ambaye ni mhariri wa gazeti la mwananchi amesema kuwa wanaliachia jeshi la polisi na kulifanyia uchunguzi tukio hilo ili hatimaye wale wote waliohusika kufikishwa katika mikono ya sheria.
Kwa upande wake Mkuregenzi mtendaji wa New Habari ambako Kibanda anafanya kazi , Hussein Bashe, amesema kuwa hivi sasa kampuni yake kwa kushirikiana na jukwaa la wahariri wanafanya jitihada za kuomba kupatiwa pass ya kusafiria ya Kibanda ili waweze kumsafirisha mpaka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Waziri wa Afya, Dr Hussein Mwinyi, ambaye nae alipata nafasi ya kumuona Kibanda, amelaani vikali tukio hilo na kuliita ni la kinyama.
Absolum Kibanda alishambuliwa kwa kuchomwa jicho la kushoto, kupigwa katika sehemu mbalimbali za mwili pamoja na kung’olewa kucha na watu wasiojulikana jana saa sita usiku akiwa anaingia nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment