Watu wapatao 200 wakiwemo
watafiti, wanasayansi na wapanga sera wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa nne wa
Afya na Sayansi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mjini Kigali, Rwanda Machi
27-29,mwaka huu.
Kauli mbiu ya mkutano huo wa
siku tatu ni : Kipaumbele cha Kanda na matarajio:’’Ushahidi wa kuchukua hatua
katika Changamoto za Mabadiliko ya Upatikana Fedha Duniani,Shirika Huru La
Habari la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti.
Mtaalamu wa
Masuala ya Afya wa Benki ya Dunia,Prof. Charles Mugone na Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Ulaya inayoshughulikia Masuala ya Afya (EDCTB) ni miongoni mwa
wataalamu watakaotoa hotuba za ufunguzi katika mkutano huo.
Mkutano huo
utakuwa na vipengele vinavyogawaanyika katika makundi manne ikiwa ni pamoja na
Afya ya Mama na Mtoto, Magonjwa yasiyo ya kuambukiza na msongo wa mawazo, Uimarishaji wa Mfumo wa Afya na Ubora wa Utoaji Huduma za Afya.
‘’EAC inafahamu umuhimu ya kuunganisha
nguvu katika kuimarsiha ushirikiano wa kikanda kwenye huduma za afya hususan
katika utafiti wa masuala ya afya,’’ alisema Katibu Mkuu wa EAC, Dr Ruchard
Sezibera.
Mkutano huo
utatanguliwa na Mkutano wa Pamoja wa Bodi za Wataalamu wa Afya na Mabaraza
utakaofanyika kati ya Machi 25 na 26, 2013 na Mkutano wa Tisa wa EAC waBaraza
la Sekta ya Afya.
Mikutano ya EAC
ya Afya na Sayansi huitishwa na Sekretarieti ya EAC na kufanyika ndani ya nchi
wanachama kwa mzunguko.
Mkutano wa kwanza
wa aina hiyo ulifanyika mjini Kampala, Uganda mwaka 2007,mkutano uliofuata
ulifanyika nchini Tanzania mwaka 2008 na nchini Kenya mwaka 2009.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment