Zaidi ya wanachama
6,000 wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii – NSSF kuanzia sasa hawana tena
sababu ya kutembelea ofisi za mfuko huo kwa ajili ya kuwasilisha michango
kutokana na kurahishwa kwa utaratibu wa uwasilishaji michango ambapo kuanzia
sasa wanaweza kufanya hivyo kupitia simu ya mkononi kwa njia ya M-pesa.
Utaratibu huo mpya
ambao unawaunganisha wanachama wa NSSF na wateja zaidi ya 10 Milioni wa kampuni ya simu ya Vodacom umezinduliwa rasmi
leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya JB
Belmonte.
“Leo tunatangaza
utaratibu mpya na rahisi ambao utawawawezesha wanachama wetu hasa walio katika
sekta isiyo rasmi kuwa na utaratibu rahisi kabisa katika historia ya
uwasilishaji michango kwa NSSF kwa njia ya simu ya mkononi ikiwezeshwa na
huduma ya M-pesa.”Alisema Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk. Ramdhani Dau.
Hata hivyo Dk. Dau
ameongeza kuwa utaratibu mpya wa uchangiaji kwa njia ya M-pesa hauufungi
utaratibu ulikokuwa ukitimika na wanachama wa mfuko huo kuwasilisha michango
yao huku vikundi na taasisi kama TUJIJENGE, TAFF, AMSHA GROUP, THT na wanachama
wengine kutoka vikundi vilivyojipanga chini ya mfumo wa uanachama wa hiari
vikitazamiwa kunufaika zaidi na mfumo mpya wa M-pesa.
Kupitia uanachama wa
hiari katika mfuko wa NSSF, kila mwanachama huchangia kuanzia Shilingi 20,000
an kuendela kwa mwezi.
“Tunataka wanachama
wetu hasa walio chini ya mfumo wa uanachama wa hiari ambao kimsingi hawana
mifuko rasmi ya akiba ya uzeeni na hivyo NSSF inawapatia nafasi ya kujiwekea
akiba wawe na njia rahisi zaidi itakayowapunguzia gharama za uwasilishaji
michango yao na hivyo kuendelea kuwekeza kwa siku za baadae.”Aliongeza Dk
Dau
Aidha, Mkuu wa Chapa
ya Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa akizungumzia huduma hii amesema kasi ya
ukuaji wa huduma ya M-pesa nchini inaendelea kuthibitisha uimara na kuaminika
kwa huduma hiyo na wadau mbalimbali.
“Kila wakati
tunaangalia ni kwa namna gani wateja wetu wanavyoweza kuitumia huduma hii
kujirahisishia maisha, ahadi yetu kwa Watanzania ni kuendelea kuiwezesha huduma
hii kuwa salama, ya uhakika na kuaminika wakati wote.”Alisema Twissa
“Tumeshawezesha
kuzileta takribani nyanja zote za huduma za biashara katika viganja vya wateja
wetu kupitia huduma hii ya M-pesa tukiwaunganisha na makampuni zaidi ya 200.
Kazi ya ubunifu bado inaendelea na wateja wetu watazidi kuona mengi zaidi
katika M-pesa ambayo uwezekano wake haukuwa rahisi hata kufikirika hapo kabla.”
Huduma ya M-pesa kwa
sasa ina mawakala zaidi ya 40,000 nchi nzima na hivyo kuifanya huduma hiyo kuwa
karibu na Watanzania mijini na vijini na kuwawezesha kufanya miamala mbalimbali
kwa urahisi na uhakika wakati wowote mahali popote.
Ili mwanachama aweze
kuwasilisha mchango wake wa NSSF kwa njia ya M-pesa anapaswa kufuata utaratibu
ufuatao katika simu yake ya Vodacom
Piga
*150*00#
Chague
nambari 4 (malipo)
Ingiza
nambari ya biashara (770770)
Ingiza
nambari ya kumbukumbu (ambayo ni nambari ya uanachama ya mwanachama)
Ingiza
kiasi cha fedha
Mwisho.
Kuhusu Vodacom Tanzania
Kampuni
ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na jamii
katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom
Foundation. Vodacom Foundation ina nguzo kuu tatu:
Afya, Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo
imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo
mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika
kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion
Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone .
Vodacom
Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania
inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Vodacom
Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo
pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited
inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35
zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom
Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa
miaka mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.
Kwa
mawasiliano:
Matina G.
Nkurlu
Meneja
Mahusiano
Vodacom
Tanzania Limited.
0 comments:
Post a Comment