Askofu Thomas Laizer
Habari
zilizotufikia hivi punde kutoka Jijini Arusha zinaarifu kuwa Askofu wa
KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Ask Thomas Laizer amefariki dunia.
Taarifa hizo zinadai kuwa Ask. Laizer amefikwa na umauti alasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha.
Jana
Februari 6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea na kumjulia
hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Taarifa
zilipasha kuwa Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya
mwezi mmoja, na hakuna daktari wala ndugu aliyekuwa tayari kusema ugonjwa
uliokuwa unamsumbua.
Pinda
alikwenda hospitalini hapo jana saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu
saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa
cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Hata
hivyo, baada ya kutoka katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi
kuzungumzia hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari
na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa
kuzungumza naye.
Awali
ilisemekana kuwa Askofu Laizer amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa
ya KCMC ya Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya watu wengi kumiminika
Selian kutaka kumwona, lakini jana ilidhihirika kuwa, amelazwa
hospitalini hapo.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu. Amen.
Via Arusha Yetu
0 comments:
Post a Comment