Waislam wametakiwa
kuwekeza katika elimu na kununua ardhi kwa maendeleo na ustawi wa jamii ya sasa
na vizazi vijavyo.
Hayo
yamesemwa na Sheikh Darwesh Kimicha wakati wa kipindi maalum cha dini ya
Kiislam cha Redio Mlimani ambapo amesema
kuna umuhimu wa kununua ardhi maalum kwa ajili ya matumizi mbalimbali na
kuachana na utegemezi.
Sheikh
Darwesh amesema kuwa kama jumuiya za kiislam zitanunua ardhi itakuwa rahisi
kwao kujenga shule,misikiti,viwanja na kumbi maalum kwa ajili ya kufanyia
shughuli mbalimbali za kiislam zikiwemo
sherehe na maadhimisho mengine.
Katika suala
la elimu amesema kuwa waislam wanatakiwa kujiendeleza katika ngazi mbalimbali
za kitaaluma na kutobweteka na maendeleo kidogo waliyo nayo
Amesema ni
wajibu wa waislam kuweka mfumo thabiti wa kutoa taaluma ya elimu anuwai ikiwemo
elimu ya ufundi kwa vijana mbalimbali wa kiislam na kuhakikisha maendeleo
yanawafikia.
Sheikh
Darwesh amesema ameanzisha mipango ya kuwasaidia vijana zaidi ya 50 eneo la Kibiti Rufiji kwa ajili ya
taaluma mbalimbali za kiufundi ili waweze kupambana na ukali wa maisha.
0 comments:
Post a Comment