Na Gideon Mwakanosya- Songea
Jeshi la polisi Mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Idd Kiambwe
Ndomondo (30) mkazi wa kijiji cha Silabu Wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara kwa
tuhuma za kukutwa na mikia ishirini ya tembo yenye thamani ya dola za
Kimarekani 300,000 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania 480,000,000.
Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa
na Kamanda wa Poliosi wa Mkoa wa Ruvuma Akili Mpwapwa zimesema kuwa tukio hilo
lilitokea Aprili 21 mwaka huu katika eneo la Biasi lililopo kata ya Nakayaya
wilayani Tunduru.
Mpwapwa alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio majira
ya asubuhi askari polisi waliokuwa kwenye kazi maalumu walifanikiwa kumkamata
mtuhumiwa Ndomondo akiwa ameficha nyara hizo kwenye begi jeusi akisafiri nazo
kuelekea Masasi mkoani Mtwara.
Alisema kuwa mtuhumiwa Ndomondo baada ya kuhojiwa na
kugundua kuwa lile begi ni la kwake walimkamata na kumrudisha Kituo Kikuu cha Polisi
cha Tunduru ambako anashikiliwa na kwamba polisi wanaendelea kumhoji zaidi.
Kamanda Mpwapwa alieleza zaidi kuwa mtuhumiwa Ndomondo
anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili mara tu
upelelezi utakapokamilika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment