WATU watatu wamefariki
dunia katika mazingira tofauti katika mkoa wa Katavi akiwemo mwanamke
aliyejinyonga kwa kanga yake mwenyewe kutokana na msongo wa mawazo uliotokana
na ugonjwa wa akili.
Ndugu Dereva Kuliwaliwa
(47) mkulima wa amepoteza mke wake, Lemi Bundala (42) aliyejinyonga kwa kanga
yake mwenyewe Oktoba 19, 2013 katika kijiji cha Kapalala wilaya ya Mlele mkoani
Katavi kutokana na kinachodaiwa kuwa ni msongo wa mawazo unaosababishwa na
maradhi ya akili aliyokuwa akiugua kwa muda mrefu.
Habari kutoka kijijini hapo
zinadai kuwa marehemu kabla ya kujinyonga alikuwa akitibiwa maradhi ya akili
katika hospitali ya wilaya ya Mpanda wakati huo huo akitibiwa kwa tiba za jadi
kijijini hapo
Inadaiwa kuwa mpaka mauti
yanamfika marehemu alikuwa akiishi kwa mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la
Marry Lubigisa (65) ambapo siku hiyo mume wa marehemu alifika nyumbani kwa mama
mkwe ili kumjulia hali mkewe ndipo mama mzazi wa marehemu aliingia katika
chumba alichokuwa akilala marehemu kwa lengo la kumuita aweze kutoka nje
kusalimiana na mumewe lakini muda huo marehemu hakuwemo chumbani kwake
Kufuatia kukosekana kwa
marehemu chumbani kwake ndugu na majirani walianza kumtafuta aliko ndipo baadae
walimkuta akiwa amejinyonga kwa kutumia kanga yake aliyokuwa akiivaa umbali wa
mita sabini kutoka nyumbani kwake.
Kaimu kamanda wa jeshi la
polisi mkoani Katavi, Emanuely Nley alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na
kueleza kuwa uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi umebaini kuwa chanzo cha
tukio kinatokana na maradhi ya akili yaliyokuwa yakimsumbua marehemu tangu
akiwa na ujauzito wa mtoto wake wa mwisho na umauti umemkuta akiendelea na
matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpanda pamoja na matibabu ya kijadi.
Katika tukio linguine
Mwinamila Dohole (50) mkazi wa kijiji cha Mnyamasi wilaya ya Mlele aliuwawa kwa
kukatwa katwa na mapanga sehemu za kichwani na kisogoni baada ya kukutwa
akiongea na mke wa ndugu Julius Lutema (38) mkazi wa kijiji hicho.
Kwa mujibu wa Kaimu kamanda
wa polisi mkoa wa Katavi, Emanuely Nnley marehemu alifikwa na mauti hayo
alipokuwa amesimama na mke wa Julius Lutema barabarani baada ya mke wa Julius
kutoka kushitaji ugomvi wa kindoa katika Serikali ya kijiji uliokuwa ukiendelea
baina yao.
Nnley alisema siku ya tukio
mke wa marehemu anayeitwa Diu Uswelu (35) alikuwa na ugomvi na mumewe ambapo aliamua
kwenda kushitaki katika serikali ya kijiji alipokuwa akirudi alisimama na ndugu
Julius Lutema ndipo walianza kushambuliana kwa mapanga na kupelekea kifo cha
marehemu na kumjeruhi mke wa marehemu ambaye alikimbizwa hospitali ya wilaya
kunusuru uhai wake.
Alisema jeshi la polisi
linamtafuta mtuhumiwa Julius Lutema ambaye alitoweka baada ya tukio ili aweze
kuchukuliwa hatua za kisheria
Akifafanua kuhusu tukio
lingine Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Katavi, Nnley alisema mnamo Oktoba 17,
2013 katika mtaa wa Nsemulwa – airtel mjini Mpanda, Isack Enock Kalinga (27)
mkazi wa Kasimba alikutwa ameuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu
ya kichwani, shingoni na kwenye mkono wa kushoto na watu wasiojulikana.
Alisema kabla ya kuuwawa
marehemu alikuwa akiishi peke yake katika nyumba yao baada ya mama yake mzazi
kumkimbia kutokana na vitisho alivyokuwa akimtishia mama yake kuwa angemuua
baada ya kushindwa kumpatia mtaji wa shilingi milioni moja.
Alisema uchunguzi wa awali
umebaini kuwa marehemu alikuwa na tabia ya ukorofi na alikuwa ametoka kifungoni
kutoka na vitendo vya ukorofi alivyokuwa akivifanya na kufungwa jela kwa
kipindi cha miezi minne kwa mara mbili tofauti ambapo bado upelelezi unaendelea
ili kuwabaini waliofanya mauaji hayo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment