Ngugi wa Thiong'o aliyepiga magoti akitunukiwa digrii ya heshima na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania mwishoni
mwa wiki kilitunuku digrii ya Heshima Mwana fasihi na mwandishi wa
vitabu maarufu Afrika Profesa Ngugi wa Thiong'o.
Ngugi alitunukiwa digrii ya Uzamivu wa Fasihi
"Doctor of Literature" ambayo ni ya pili kutunikiwa barani Afrika baada
ya aliyotunikiwa kutoka Chuo Kikuu cha Walter Sesulu cha Afrika ya
Kusini.
Raia huyo wa Kenya ambaye aliwahi
kukimbilia uhamishoni baada ya maandiko yake kupingana na serikali ya
Kenya sio mgeni nchini Tanzania kwani baadhi ya vitabu vyake
vimeorodheshwa katika mitaala ya shule za sekondari na vyuo vya elimu ya
juu nchini humo.
Akizungumzia kuhusu heshima hiyo aliyopewa na
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ngugi amesema amefurahishwa kwa kuwa Chuo
hicho kikuu kimetambua mchango wake katika fani ya fasihi na uandishi wa
vitabu.
Akizungumzia kuhusu waandishi vijana
wanaochipukia Ngugi amesema amefurahishwa kuona na baadhi ya waandishi
vijana ambao wanafuata nyayo zao kwa kuandika mambo yanayogusa jamii na
kuibua mambo mazito.
Kuhusu maono ya kuandika kitabu kitakachohusu
matukio yaliyotokea Kenya hivi karibuni Ngugi amesema anatafakari na upo
uwezekano akaandika kitabu kinachohusu hayo yaliyotokea.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment