Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Februari 10,
2013 amekabidhi pikipiki aina ya bajaj kwa mama mmoja mlemavu, Mama Sarah
Mkumbo Nalingigwa katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu Ndogo mjini Dodoma.
Mama Nalingigwa ni
mtumishi wa Wakala wa Barabara nchini – TANROADS- katika Mkoa wa Singida na
shughuli hiyo imehudhuriwa pia na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa John Pombe
Magufuli, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mufugale na Mama Salma
Kikwete.
Shughuli ya
makabidhiano ya leo, inatimiza ahadi ambayo Mheshimiwa Rais aliitoa kwa Mama
Nalingigwa wakati alipokutana naye miongoni mwa wananchi waliohudhuria sherehe
ya utiaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Barabara ya Manyoni-Itigi=Chaya mjini
Itigi, Mkoa wa Singida Novemba mwaka jana.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhi pikipiki hiyo, Rais Kikwete amemwambia mama huyo:
“Nimefurahi kwamba nimeweza kutimiza ahadi yangu. Hii ndiyo faraja yangu kwamba
sasa utaweza kufanya kazi zako kwa urahisi zaidi, utaweza kutembea kwa urahisi
zaidi na kufika kazini na kurejea nyumbani kwa namna ya haraka zaidi.”
Naye Mama Nalingigwa
amewwambia Rais Kikwete: “Wewe ni kiongozi shupavu, kiongozi hodari na
mpiganaji anayemjali kila mtu. Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu akujalia ili uendelee
kuwaona wengine wenye mahitaji kama ya kwangu.”
Ameongeza mama huyo
ambaye amefanya kazi Wizara ya Ujenzi kwa miaka 30 iliyopita: “Kwa kuniwezesha
kiasi hiki, umenipa uwezo wa kufanya kazi kwa namna bora zaidi., Ni vyema kuwa
viongozi wengine wakaiga mfano wako wa kujali watu walioko chini yako.”
Amesisitiza: “ Sisi
walemavu tuna mahitaji mengi na hivyo naomba unedelea kutuangalia kwa jicho la
huruma na kutupunguzia vikwazo vya maisha kila nafasi inapojitokeza.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment