Timu ya taifa ya Afrika Kusini imeondolewa na Mali katika mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mikwaju ya penati 3-1.
Katika mikwaju hiyo, Mali walifunga penati zote 3 walizopiga na kuwafanya waibuke washindi wakati Afrika Kusini ilipata penati moja kati ya 4 zilizopigwa lakini ilikosa penati tatu.
Penati hizo zilipigwa baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika dakika 90, zilipoongezwa dakika 30 hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake.
Awali kulikuwa na mchezo mwingine kati ya Ghana na Cape Verde ambapo Ghana imeweza kutoka kifua mbele kwa mabao 2-0.
Kwa matokeo hayo Ghana na Mali zimetinga nusu fainali zikisubiri washindi wa michezo ya kesho ambapo Ivory Coast itaumana na Nigeria wakati Togo itacheza na Burkina Faso.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment