Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia, Bwana Justin Yifu Lin, Ijumaa wiki hii Februari mosi, 2013 Ikulu, Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa China katika Tanzania Mheshimiwa Lu Youqing.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini baada ya kuthibitisha maelezo yake
binafsi kwenye Fomu ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za
kupatiwa Kitambulisho hicho nyumbani kwake jijini Dar es salaam leo, Ijumaa, Februari
Mosi, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) Bwana Dickson E Maimu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha kwa ajili ya Kitambulisho cha
Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa
nyumbani kwake asubuhi ya jana, Ijumaa, Februari Mosi, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akichukuliwa alama za vidole wakati alipokamilisha
taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa nyumbani kwake asubuhi ya jana,
Ijumaa, Februari Mosi, 2013.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment