Abiria mmoja (mwenye tisheti nyeupe) aliyekuwa akisubiria daladala
katika kituo cha mabasi cha mwenge Dar es Salaam akizozana na kondakta
na mpiga debe baada ya kukataa kulipisha basi linalofanya safari kati ya mwenge na Posta,aliwagomea akidai basi haliruhusiwi kupanda juu ya
vikingo vya barabara kwa madai ni sehemu ya abiria kusimama. Mara nyingi
madereva katika kituo hicho wanakatiza licha ya kutotakiwa kufanya
hivyo.
Hatimaye kondakta na mpiga debe wakamburuta abiria huyo na kumuweka
pembeni ili kuruhusu gari lao kupita kwenye kingo za barabara kinyume cha sheria.
Ajali Nyingine
Ukiwa mjasiriamali tambua fursa hapa picha zinaonekana zinauzwa
ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo wahusika walipigwa wakiwa kwenye
mkutano mkuu wa wakaguzi wa hesabu za serikali,wanalazimika kukomboa
picha moja kwa kati ya shilingi elfu tatu na elfu tano ingawa baadhi
walilalamika kuwa walipigwa bila ya ridhaa hivyo kulazimika kuongeza
bajeti. Picha nyingi malipo zaidi.
Nani alikwambia siasa haina uhusiano na biashara? hapa ni nje ya
hotel Blue Pearl mkutano wa CHADEMA ulikuwa ukiendelea kufanyika ndani
lakini nje kuna vijana wanauza bidhaa mbalimbali zenye nembo ya
chama kama vile fulana,kofia, Skafu,mashati,DVD,CD na kadhalika.
Biashara
ni popote,vijana wakiwa wamehamishia biashara zao nje ya chuo cha
kodi,maeneo ya Mwenge jijini wakati wa shughuli za mahafali zilizofanyika
hivi karibuni,kama wanavyoonekana vijana wanauza mashada ya maua,mapambo
mengine muhimu kwa shughuli kama hiyo.
Kama kuna kero inayowasumbua wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni uwepo
wa kunguru weusi maarufu kunguru wa Zanzibar,katika kukabiliana na hilo
baadhi ya wakazi na taasisi wanaweka mitego kama inayooneka kwenye picha
ili kuwanasa kunguru hao kwa kuwawekea vivutio ndani kama mabaki ya
chakula kwa kawaida wakiingia hawawezi kutoka katika mtego huu.Hapa ni
chuo cha cha biashara CBE.
Kunguru wa Zanzibar sio waoga kama wale wa bara wenye baka jeupe huwa wana uwezo wa kukwapua kitu kama vile andazi ama mnofu wa nyama ama kipande cha samaki na kuondoka nacho.
Kunguru wa Zanzibar sio waoga kama wale wa bara wenye baka jeupe huwa wana uwezo wa kukwapua kitu kama vile andazi ama mnofu wa nyama ama kipande cha samaki na kuondoka nacho.
Shuhuda
mmoja mkazi wa Tandale jijini Dar es Salaam anasimulia kuwa aliwahi
kupigana na mke mwenzake baada ya kunguru kuhamisha nguo ya ndani kutoka
kwake mpaka bafu la mwanamke mwenzake huyo hivyo wakalihusisha na
ushirikina hata hivyo wanafunzi waliomuona kunguru akifanya vituko hivyo
walisaidia kutanzua mgogoro huo vinginevyo ingekuwa balaa.
Picha na Gervas Charles Mwatebela
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Picha na Gervas Charles Mwatebela
0 comments:
Post a Comment