![]() |
| Kikosi cha Taifa Stars |
![]() |
| Mbwana Samata Akishangilia moja ya magoli yake. |
Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia
uliochezwa jana (Januari 11, 2013)
kwenye Uwanja wa Addis Ababa hapa jijini
Addis Ababa, Ethiopia.
Taifa Stars inarejea nyumbani LEO ambapo
itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki mmoja wa Ethiopia.
Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.
Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment