ROONEY KUIKOSA LIVERPOOL
Wayne Rooney
Mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney ataikosa mechi dhidi ya mahasimu wao Liverpool katika mechi ya ligi kuu kutokana na maumivu ya goti yanayomsumbua.

Kocha wa timu hiyo Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa kwamba mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza atakuwa fiti zaidi kwa mechi ya jumatano dhidi ya West Ham United.

Hata hivyo kocha huyo amefarijika kwa kiasi fulani kutokana na kurejea kwa Anderson na Luis Nani waliokuwa majeruhi hivyo wataikaribisha  Liverpool siku ya jumapili katika uwanja wa Old Trafford,jijini Manchester .


Wakati wa Man United wakiwakaribisha mahasimu wao wakiongoza ligi kuu (pointi 52) kwa tofauti ya pointi 21 dhidi ya Liverpool ambao wako nafasi ya 8 kwa pointi zao 31.

DIEGO MILITO KUREJEA DIMBANI
Diego Milito
Mshambuliaji mkongwe wa Inter  Milan ya Italia anataraji kurejea dimbani wikiendi hii baada ya kupona majeraha ya goti yaliyokuwa yakimsumbua.
Milito (33) mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anataraji kukipiga katika mechi ya leo ligi kuu nchini Italia serie A dhidi ya Pescara.
Inter Milan bado inapambana kuhakikisha inarejesha heshima msimu huu kwani mpaka hivi sasa ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 35,pointi TISA nyuma ya vinara wa ligi hiyo Juventus wenye pointi 44.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top