![]() |
| Yaya Toure. |
![]() |
| Gervais Lombe Yao Kouassi (Gervinho). |
Klabu za ligi kuu nchini England zitaanza kuonja shubiri ya kuwakosa nyota wake kutoka Afrika ambao wanazitumikia timu zao za Taifa katika michuano ya mataifa Afrika huko Afrika Kusini.
Tembo wa Afrika, Ivory Coast
inaonekana ni timu ya taifa ambayo itaziathiri timu nyingi za ligi kuu nchini
England kwani ina wachezaji wengi zaidi kuliko nchi nyingine zinazoshiriki
michuano hiyo.
Mabingwa watetezi wa ligi
hiyo Manchester City wataanza kuzikosa huduma za Yaya na kaka yake Kolo Toure
ambao wanaitumikia Ivory Coast huko bondeni katika michuano hiyo itakayoanza
kutimua vumbi Januari 19 hadi Februari 10 mwaka huu.
Kocha Msaidizi wa Man City David
Platt amesema kuwa hawajui Yaya na Kolo Toure watafika hatua gani lakini
wanajua jinsi ya kufanya ili kuziba nafasi zao.Suala hili ni sawa na wanapokuwa majeruhi wa muda mrefu tunawakosa
uwanjani,lakini wangekuwepo walikuwa muhimu kikosini.Mwaka Yaya Toure hakuwepo
kikosini lakini tulichukua ubingwa wa ligi kuu England’’ aliongeza kocha huyo.
Wanaijeria Obi Mikel na
Victor Moses watajiunga na Super Eagles na kuachana na kibarua chao Stamford
bridge makao makuu ya Chelsea kwa muda kupisha shamrashamra za michuano ya mataifa ya Afrika.
Newcastle United itamkosa mchezaji wake tegemeo Cheikh Tiote huku Washika bunduki wa London Arsenal
wakimkosa mchezaji Gervinho ambaye anakwenda kuitumikia Ivoryo Coast
inayoshiriki katika michuano hiyo katika kundi D la Algeria,Tunisia na Togo.
Aruna Kona wa Ivory Coast
naye atatengana na klabu yake ya Wigan Athletics kwa ajili ya michuano hiyo
yenye msisimko mkubwa barani Afrika.
Naye Kocha wa Morocco Rachid
Taoussi Adel amewaita kikosini Taarabt Marouane Chamackh ambaye anaitumikia
West Ham kwa mkopo akitokea Arsenal.
Tottenham itamkosa
mshambuliaji wake wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor, huku kocha Andres
Villas Boas akisema wataheshimu uamuzi wa Adebayor kama ataamua kuichezea Togo
au kubakia White Hart Lane.
Hata hivyo kukosekana
Senegal maarufu kama Simba wa Teranga kunatoa nafuu kwa makocha kama Rafael
Benitez wa Chelsea ambaye atamtumia mchezaji wake mpya Demba Ba huku kocha
Newcastle akimtumia pacha wake Papis Cisse.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI


0 comments:
Post a Comment