Kikosi Cha timu ya Taifa Stars
Timu ya taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu Taifa Stars inataraji kushuka ugani saa 11.30 kwa saa za Afrika ya Mashariki katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.  

Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa Machi mwaka huu.

 Mechi hiyo itakuwa kipimo cha mwisho kwa Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.

Ethiopia iko kundi C pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina Faso. Ethiopia itacheza mechi yake ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Zambia.

Katika mechi yake ya mwisho, Taifa Stars iliifunga Zambia bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Desemba 22 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa Machi mwaka huu.
 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Top