SERGIO RAMOS AFUNGIWA MECHI TANO
Sergio Ramos
Beki Sergio  Ramos wa klabu ya Real Madrid amefungiwa mechi tano na shirikisho la soka nchini Hispania baada ya kutolewa na kadi nyekundu  kumtukana mwamuzi wakati timu yake ikicheza dhidi ya Celta vigo.
Hata hivyo ni pigo kubwa kwa kocha wa Real Madrid Jose Mourinho ambaye ana pengo la beki wake Mreno Pepe ambaye ni majeruhi.Mabeki wengine Marcelo na Fabio Coentrao.
Hata hivyo Real Madrid ilishinda mechi hiyo kwa magoli 4 – 0 na kutinga hatua ya 16 bora.

NEYMAR BADO YUPO YUPO KWANZA
Neymar Santos
Nyota  wa klabu ya Santos na timu ya taifa ya Brazili,NEYMAR amesema kuwa hana mpango wa kuhamia klabu za Ulaya kwa sasa.
Neymar(20) mchezaji bora wa Amerika kusini amesema lengo lake ni kuisaidia SANTOS na timu ya taifa ya Brazili.
 Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa klabu kubwa Ulaya zikiwemo,AC Milan,Real Madrid,Chelsea na Manchester City.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top