Katibu Mkuu Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Joyce Ndalichako
 Watahiniwa wa mtihani wa kidato cha sita 2013 watafanya mtihani wa kuhitimu masomo yao mwezi Februari mwaka huu. Hii ni tofauti na ilivyotangazwa katika mabadiliko ya mihula yaliyofanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo walipaswa kufanya mitihani yao mwezi Mei. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika mtandao wao.

Baraza hilo linasisitiza kuwa mabadiliko hayo hayawahusu watahiniwa wa mtihani kidato cha sita mwaka 2013.

“Mabadiliko ya mihula yaliyofanywa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yataanza kutumika kwa Watahiniwa wa Kidato cha Nne mwaka 2013, ambao watafanya mtihani wao mwezi Novemba na Watahiniwa wa Kidato cha Sita mwaka 2014 ambao watafanya mtihani wao mwezi Mei” inasema taarifa hiyo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top