Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ndugu Philip Mulugo
Matokeo ya kidato cha pili yametangazwa ambapo yanaonesha kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asimilia 19.15 kwa mwaka jana ukilinganisha na matokeo ya mwaka wa 2011.
 

WANAFUNZI WALIOSHIKA NAFASI 10 BORA NI 1.Magreth Kakoko 2.Queen Masiko wote kutoka St.Francis ya Mbeya,3.Lukundo Manase na Frank Nyantarila kutoka Kaizirege sekondari za mkoani Kagera,Grace Msovella,Harieth Makiriye,Robinnacy Mtitu kutoka St Francis-Mbeya,Muhsin Hamza na Annastazia Kabelinde kutoka Kaizirege ya Kagera.
 

SHULE 10 ZA SERIKALI ZILIZOFANYA VIZURI
1.MZUMBE 2.TABORA WAVULANA 3.ILBORU 4.KIBAHA 5.IYUNGA 6.KIBAHA
7.MALANGALI 8.IFUNDA-UFUNDI 9.SAMORA MACHEL 10.KILAKALA.
 

SHULE 10 ZA BINAFSI ZILIZOFANYA VIZURI
1.KAIZIREGE 2.MARIAN WAVULANA 3.ST.FRANCIS 4.DON BOSCO 5.BETHEL SABS
6.MARIAN WASICHANA 7.DON BOSCO (MOSHI) 8.CANOSSA 9.ST JOSEPH
ITERAMBOGO SEMINARY 10.CARMEL

SHULE 10 ZA SERIKALI  ZILIZOFANYA VIBAYA ZAIDI
1.MIHAMBWE 2.DINDUMA 3.KIROMBA 4.MARAMBO 5.MBEMBALEO 6.KINJUMBI
7.LITIPU 8.LUAGALA 9. MIGURUWE 10.NAPACHO
 

SHULE 10  BINAFSI ZILIZOFANYA VIBAYA ZAIDI
1.MFURU 2.PWANI 3.DORETA 4.KIGURUNYEMBE 5.RURUMA 6.AT-TAAUN 7.JABAL
HIRA SEMINARY  8.MKONO WA MARA 9.KILEPILE 10.KIUMA.


Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Phillip Mulugo amesema kuwa jumla ya watahiniwa LAKI MBILI ELFU AROBAINI NA TISA NA MIATATU ISHIRINI NA TANO (249, 325) sawa na asilimia 64.55 huku watahiniwa LAKI TATU ELFU THEMANINI NA SITA NA MIAMBILI SABIBI NA MOJA (389, 271) wamefuzu kuingia kidato cha tatu. Wanafunzi 136,923 ambayo ni sawa na asilimia 35.4 wamefeli mtihani huo wakiwemo wasichana elfu sabini na nne na ishirini (74,020) na wavulana elfu sitini na mbili na mia tisa na tatu (62, 903).
 

Waziri Mulugo amesema kuwa watahiniwa 23 wamefutiwa matokeo kwa tuhuma za  kujihusisha na vitendo vya udanganyifu ambapo watalazimika kurudia kidato cha pili mwaka 2013.

Wanafunzi SITA kutoka shule ya St Francis ya Mbeya  wamekuwa miongoni mwa watahiniwa KUMI BORA katika mtihani huo wakati wanafunzi wanne wakitoka shule ya Kaizirege ya mkoani Kagera.
 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top