36
WACHUKUA FOMU TFF, 18 WAREJESHA
Wakati
kesho ndiyo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye
uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari wamesharejesha.
Idadi
hiyo ni kufikia leo mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya
TFF inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email wanatakiwa kuzituma kwa
Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya tfftz@yahoo.com na si
kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.
Waombaji
wanne walioongezeka katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na
Rukwa, Eliud Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na
Omari Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha
kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo
(urais) wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura,
Ramadhan Nassib na Wallace Karia.
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum
Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na
Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra
Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise
(Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy
Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James
Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima
(Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki (Morogoro na
Pwani), Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed
(Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda
(Dar es Salaam).
Kwa
upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili
tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu
ya kuwania umakamu mwenyekiti.
SUPER
WEEK TENA NDANI YA LIGI KUU YA VODACOM
Mzunguko
wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa na
maombi ya televisheni ya SuperSport kuonesha mechi za Super Week kama
ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
Raundi
tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati
nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.
0 comments:
Post a Comment