Hen Kijo Bisimba
Watanzania wametakiwa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni hatari kwa mustakabali wa amani na utulivu  wa nchi ya Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu Dakta Hellen Kijo Bisimba  kimelaani mauaji ya kikatili dhidi ya  polisi wawili huko mkoani Kagera.
Mkurugenzi huyo ameiomba serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya waliohusika katika tukio hilo la kinyama.
Dakta Kijo Bisimba amesema kituo chake kinatoa pole kwa Jeshi la Polisi kwa kupoteza nguvu kazi ya taifa ambayo bado ilikuwa inahitaji kwa wakati huu.
Tayari Ispekta mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema ameunda timu maalum ya uchunguzi toka makao makuu itakayounga na timu ya mkoa wa Kagera kuchunguza tukio hilo.

CHADEMA KATIBA HAITAPATIKANA KABLA YA 2015
Serikali imetakiwa kufanya mabadiliko makubwa  ya sheria ya tume ya taifa ya uchaguzi na sheria ya uchaguzi bila kujali mchakato wa mabadiliko ya  katiba
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo  CHADEMA Freeman Mbowe amesema pia kunatakiwa tume huru ya uchaguzi ambayo itafanya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 uwe huru na haki.
Kiongozi huyo amesema kuwa huenda mabadiliko ya katiba yasifanyike kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015 hivyo mabadiliko ya sheria zilizopitwa na wakati ni muhimu bila kujali  kukamilika kwa mchakato wa katiba.
Bwana Mbowe amesema mabadiliko ya uchaguzi yasipofanyika kutatoa taswira tofauti hivyo angalizo ni kufanya mabadiliko kwani wananchi wamechoka kuyumbishwa na tume ya uchaguzi ambayo amedai siyo huru.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top